19 Machi 2011 - 20:30

Asasi za kutetea haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeonya kuhusiana na machafuko ya uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi ujao ambapo kampeni zake zilianza rasmi usiku wa kuamkia jana

Ripoti ya Shirika la Habari la AhlulBayt(a..s)ABNA:Makundi hayo ya haki za binadamu yamewatuhumu wagombea wa uchaguzi huo kwamba, wamezusha anga ya hofu na woga. Asasi za kutetea haki za binadamu za Congo na zile za kimataifa zimewatumia barua wagombea wa kiti cha Urais wakiwataka kuendesha kampeni zao kwa amani na utulivu na kujiepusha na hotuba za uchochezi. Aidha barua hiyo imewataka wagombea Urais kujiepusha na hotuba za ukabila na kashfa. Hayo yanajiri katika hali ambayo, mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia vurugu zilizojitokeza wakati wa ufunguzi wa kampeni hizo. Uchaguzi wa Bunge na Rais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umepangwa kufanyika tarehe 28 ya mwezi ujao wa Novemba.